SHIRIKISHO
la Soka Tanzania, (TFF) limeikomalia klabu Yanga kuheshimu katiba na
kuahakikisha wanafanya uchaguzi mapema.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana,Rais wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi alisema Yanga waliwaandikia barua Agosti,
2015 wakiomba kuahirisha uchaguzi ili kupisha Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge
uliofanyika Octoba 30, 2015 lakini hadi sasa wamekaa kimya.
“Kati ya wanachama
44 wa shirikisho hilo hakuna mwanachama anayemzidi mwenzake hivyo Yanga kuacha
kufanya uchaguzi ni kuvunja katiba ya TFF, CAF na FIFA hivyo nitahakikisha
uchaguzi wa Yanga unafanyika mapema iwezekanavyo”, alisema Malinzi
Kauli ya TFF
imekuja baada ya muda wa kukaa madarakani kikatiba kumalizika toka June 2014 na
kuongezewa mwaka mmoja na mkutano Mkuu wa wanachama ili kufanya marekebisho ya
katiba ya klabu hiyo lakini hadi sasa wapo
kimya.
Mapema wiki hii,
Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro alisema uongozi wa klabu hiyo umemchagua
Wakili Sam Mapande kuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi.
Mapande amechukua
nafasi ya Alex Mgongolwa aliyejiuzulu kutokana na kuwa na majukumu mengine na
kwamba Mwenyekiti huyo ataitisha kikao cha Kamati ya Uchaguzi na ndicho
kitakachokuwa na jukumu la kupanga tarehe ya uchaguzi wa Yanga
No comments:
Post a Comment