Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Asia (AFC), na Makamu wa Rais wa FIFA, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa leo ametembelea ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) zilizopo Karume jijini Dar es salaam.
Sheikh Salman alifika katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) akiwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambapo alikutana na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanya na shirikisho, ikiwemo uwanja wa Karume, na Hostel zilizopo Karume.
Kiongozi huyo wa AFC, aliwasali nchini jana mchana kwa matembezi ya siku mbili chini ya mwenyeji wake Rais wa TFF, Jamal Malinzi na anatarajiwa kuondoka nchini kesho.
No comments:
Post a Comment