BOSI wa TP Mazembe, Moise Katumbi,
amemfuata straika wake, Mbwana Samatta nchini Ubelgiji ili kuweka mambo
sawa ili mchezaji huyo ajiunge na Klabu ya KRC Genk.
Samatta
alitangulia kwenda Ubelgiji ambako alifika juzi Alhamisi na kukutana na
wakala wake ambaye walianza kukamilisha taratibu za mchezaji huyo
kujiunga na klabu hiyo, lakini Samatta, jana alitambulishwa rasmi
klabuni hapo baada ya kusaini mkataba wa miaka minne na nusu.Katumbi yeye anawasili Ubelgiji, leo Jumamosi kuungana na Samatta na wakala wake kukamilisha baadhi ya mambo licha usajili wa mchezaji huyo kuwa umekamilika.Viongozi wa Klabu ya KRC Genk wakimtambulisha Samatta.
“Katumbi amefika leo (jana) na alijiunga na Samatta kukamilisha mambo ya msingi na viongozi wa Genk na mambo yapo sawa, yaani Samatta ni mali ya Genk,” alisema ofisa huyo.
Tovuti ya Genk pia iliandika jana kuwa, Samatta tayari ni mchezaji wao na anaweza kutumika muda wowote.
Awali Katumbi alionekana hataki Samatta ajiunge na Genk kutokana na klabu hiyo kutotumia njia sahihi katika kumsainisha mkataba wa awali bila kuwasiliana na TP Mazembe.
No comments:
Post a Comment