Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 5, 2016

REAL MADRID YAMTIMUA RAFAEL BENITEZ, ZINEDINE ZIDANE KUCHUKUA TIMU

Ni baada ya Miezi saba tuu ya Uongozi wake
HABARI ZA MAPEMA KABLA
Benitez, ambae amedumu Miezi 7 tu katika Mkataba wake wa Miaka Mitatu, atafukuzwa na Lejendari Zinedine Zidane kutwaa wadhifa huo.
Hivi sasa Zidane ndie Kocha wa Kikosi cha Real Madrid B.
Jana Real ilitoka Sare 2-2 na Kikosi cha Gary Neville, Mchezaji wa zamani wa Man United ambae sasa anaifundisha Valencia, iliyotoka 2-2 na Real Uwanjani Mestalla katika Mechi ya La Liga, Sare ambayo imewaacha Vigogo hao Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Atletico Madrid.
Tangu atue Real, Benitez amekuwa si kipenzi cha Mashabiki wa Klabu hiyo, na kutandikwa 4-0 kwenye El Clasico Mwezi Novemba na Mahasimu wao Barcelona hakukumsaidia hata kidogo.

Pia kutupwa nje ya Copa del Rey baada ya kumchezesha Mchezaji asiestahili katika Mechi na Cadiz kumechochea chuki dhidi yake.

Hali hiyo imefanya kuwepo minong’ono ya kila mara kuwa Wachezaji wa Real hawana raha na Benitez na wana mgomo baridi dhidi yake.
Wiki iliyopita Benitez aliwatuhumu Wanahabari kwa kuendesha kampeni kumpinga yeye, Klabu na Rais wao Florentino Peréz.