Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 5, 2016

LIVERPOOL WASAINI MCHEZAJI

MENEJA wa Liverpool Jurgen Klopp yupo hatua za mwisho kukamilisha usajili wake wa kwanza wa Mchezaji mpya na huyo ni Marko Grujic.
Grujic, mwenye Miaka 19, Leo ametua Anfield kwa upimwaji wake wa afya ili kukamilisha Dili ya Pauni Milioni 5.1 kutoka Red Star Belgrade.
Inatarajiwa baada ya kukamilika kwa Uhamisho wake kwenda Liverpool, Kinda huyo atarudi kuichezea kwa Mkopo Red Star hadi mwishoni mwa Msimu na kujiunga na Liverpool kwa ajili ya Msimu ujao.
Liverpool imelazimika kufanya uamuzi wa kumnunua Grujic hivi sasa kwa sababu alikuwa akiwindwa pia na Klabu za Russia, CSKA Moscow na Zenit St Petersburg, ambazo zilitoa Dau kubwa, ikiaminika kuwa ni zaidi ya Pauni Milioni 7.

Lakini Kijana huyo aliamua mwenyewe kujiunga na Liverpool baada ya Msaidizi wa Klopp, Zeljko Buvac, ambae anatoka Serbia, kuingiliwa kati na kuleta ushawishi mkubwa kumchota Kijana huyo anaechezea Timu ya Taifa ya Serbia ya U-21.