MUME wa Celine Dion ambaye pia ni mwanamuziki René Angélil, amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 73.
Amekufa kutokana na ugonjwa wa kansa limeandika Us Weekly.
"René Angélil, 73, amefariki dunia leo asubuhi nyumbani kwake Las Vegas baada ya mapambano ya muda mrefu na ugonjwa wa kansa," taarifa kwa Us ilisema.
"Familia inaomba kwamba wakati wa maombolezo hayo kwa sasa faragha yao lazima iheshimiwe."
Angélil ambaye alizaliwa Montreal alianza muziki miaka ya 1960 na baadae akaanza kufanya shughuli za kumeneji wasanii akiwamo Celine Dion.
Wawili hao walioana 1994 muda mfupi kabla ya Celine kutoka na wimbo ulitumiwa katika filamu ya Titanic wa "My Heart Will Go On ”.
Dion na mume wake wamepata watoto watatu mkubwa akiwa ni René-Charles, 14, na mapacha Nelson na Eddy wakiwa na miaka na 5.
No comments:
Post a Comment