Mfungaji
bora na hatari wa Ligi Kuu England Jamie Vardy ameripotiwa kuwa atakuwa
nje ya Uwanja kwa Wiki 2 baada ya kufanyiwa operesheni ndogo ya Nyonga.
Vardy, mwenye Miaka 28 na ni Straika hatari wa Leicester City, ndie anaefungana na Romelu Lukaku kwa Ufungaji Mabao katika Ligi Kuu England wote wakiwa na Magoli 15 kila mmoja.
Vardy ndie ameibeba Leicester City kuwa juu kwenye Ligi Kuu England wakiwa Nafasi ya Pili Pointi 2 nyuma ya Vinara Arsenal na Msimu huu ameweka Rekodi kwenye Ligi hiyo kwa kufunga Mabao katika Mechi 11 mfululizo za Ligi.
Lakini tangu aweke Rekodi hiyo, Vardy amefunga Bao 1 tu katika Mechi 6 zilizopita.
Ukame huo umeifanya Leicester ipokonywe uongozi wa Ligi baada ya kushindwa kufunga katika Mechi 3 na kuambua Pointi 2 tu katika hizo. Wikiendi ikayo hamna Mechi za Ligi na badala yake zipo Mechi za FA CUP na Leicester watakuwa Nyumbani kucheza na Tottenham.

No comments:
Post a Comment