Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, January 6, 2016

WAYNE ROONEY MCHEZAJI BORA ENGLAND 2015, AZOA TUZO MARA YA PILI MFULULIZO

KEPTENI wa Manchester United, Wayne Rooney, ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa 2015 akitetea tena Tuzo ambayo pia aliipata 2014.
Hii ni mara ya 4 kwa Rooney kuzoa Tuzo hii ambayo Wachaguaji wake ni Masapota wa Timu ya Taifa ya England.
Mapema Desemba England ilianika Listi ya Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Nchi yao ambapo pia ipo Tuzo kwa Chipukizi Vijana wa chini wa Miaka 21, U-21.
Kepteni wa England, Wayne Rooney, ambae alishinda Tuzo hiyo Mwaka Jana, ni miongoni mwa Wachezaji Watano waliokuwa wakiigombea.

Rooney Mwaka 2015 aliiongoza England kufuzu kuingia Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, ambazo zitachezwa huko France Mwezi Juni huku akihakikisha England inashinda Mechi zao zote 10 za Kundi lao na kuifungia Jumla ya Bao 5 kwa Mwaka 2015 kwa England huku pia akiivunja Rekodi ya Sir Bobby Charlton ya Ufungaji Bora katika Historia ya England kwa kufunga Bao 50 Rekodi ambayo iliwekwa na Charlton Mwaka 1968 alipofunga Bao lake la 49.