Klabu ya soka ya Chelsea ya nchini England imeongeza jina la mshambuliaji wa klabu ya soka nchini Italia AC Milan, raia wa Colombia Carlos Bacca mwenye miaka 29 katika orodha ya wachezaji inaowahitaji kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.
Carlos Bacca aliyejiunga AC Milan akitokea klabu ya Sevilla ya nchini Hispania, anaweza kuihama klabu hiyo kutokana na mwenendo wake wa kusuasua kwenye ligi ambapo AC Milan inashika nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi huku wakiwa nyuma ya vinara Napoli kwa points 12.
Chelsea ambayo ilimfuta kazi kocha Jose Mourinho mwezi uliopita na kumpa mkataba wa muda mholanzi Guus Hiddink inataka kukiongezea nguvu kikosi chao katika vita waliyonayo ya kujisikuma kupanda kutoka chini wakiwa nafasi ya 14.
Guus Hiddink anataka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji ambayo hadi sasa inaongozwa na Diego Costa, Loic Remmy na Radamel Falcao ambao wote wanaonekana hawana makali yale ya kuisukuma Chelsea kwa nguvu zote.
No comments:
Post a Comment