LIONEL MESSI Usiku huu ametunukiwa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2015 iitwayo FIFA Ball d’Or huko Zurich, Uswisi katika Hafla maalum.
Messi, Straika wa Barcelona na Kepteni wa Timu ya Taifa ya Argentina, amewabwaga Cristiano Ronaldo, alietwaa Tuzio hii kwa Miaka Miwili mfululizo iliyopita, na Neymar.
Hii ni mara ya 5 kwa Messi kutwaa Tuzo hii na kuweka Historia baada ya pia kuitwaa kuanzia 2009 hadi 2012.
Pamoja na Messi, Kocha wa Barcelona, Luis Enrique, nae ametwaa Tuzo ya Kocha Bora Duniani kwa Mwaka 2015 kwa kuiwezesha Barcelona kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa La Liga, Copa del Rey na UEFA CHAMPIONS LIGI.
WASHINDI 2015:
FifPro World XI [Kikosi Bora Duniani:
-KIPA: Manuel Neuer [Bayern Munich]
-MABEKI: Thiago Silva (PSG), Marcelo (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Dani Alves (Barcelona)
-VIUNGO: Andres Iniesta (Barcelona), Luka Modric (Real Madrid), Paul Pogba (Juventus)
-MAFOWADI: Neymar (Barcelona), Leo Messi (Barcelona), Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
Kocha Bora Kinamama:
-Jill Ellis [USA]
Kocha Bora:
-Luis Enrique [Barcelona
Uchezaji wa Haki:
-Klabu zote zinazosaidia Wakimbizi
Tuzo ya Puskas [Goli Bora]:
- Wendell Lira [Atletico Goianiense ya Brazil]
Mchezaji Bora Kinamama:
-Carli Lloyd [USA]
wa Haki:
No comments:
Post a Comment