MABINGWA
watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Yanga kesho wanaingia uwanjani kuwakabili
Lipuli FC ya Iringa katika mchezo wa wao wa kwanza wa ligi hiyo utakaofanyika
kwenye Uwanja wa Uhuru.
Yanga
itaendelea kuwakosa nyota wake Obrey Chirwa na Pius Buswita kutokana na kesi
tofauti, ambapo Buswita amesimamishwa mwaka mmoja baada ya kubainika kusaini
mara mbili Simba na Yanga.
Chirwa licha
ya kuwa ni majeruhi lakini pia, alisimamishwa na Kamati ya Usimamizi ya
Uendeshaji Bodi ya ligi ile ya masaa 72 ya msimu uliopita baada ya kumpiga
mwamuzi Ludovic Charles katika mchezo wa kumaliza msimu dhidi ya Mbao FC hivyo,
anasubiri suala lake kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Yanga
imekuwa haitabiriki katika mechi zake za mwanzo kuna wakati huanza vibaya na
wakati mwingine huanza vyema. Lakini mara nyingi imekuwa ikifanya vizuri katika
mechi za nyumbani.
Lipuli ni timu iliyopanda msimu huu na ina kocha
mzoefu wa ligi Seleman Matola ambaye anaifahamu Yanga vizuri. Hautakuwa ni mchezo rahisi kwa kila
mmoja ingawa Yanga inaweza ikapewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na aina ya
kikosi ilichosajili msimu huu.
Baadhi ya
nyota wa Yanga waliong’ara katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba
JUmatano, Ibrahim Ajib, Donald Ngoma, Gadiel Michael, Thaban Kamusoko na Papy
Kabamba Tshishimbi wanatarajiwa kuendeleza makali yao iwapo watapangwa.
Lakini sio
mchezo wa kudharau hasa Lipuli FC kwani wanajua wanakutana na timu ya aina gani
hivyo, watacheza kwa juhudi kujionyesha kuwa hata wao ni bora.
Kocha wa
Yanga George Lwandamina alisema maandalizi yanakwenda vizuri na wamejipanga
kuhakikisha pointi tatu zinabakia kwao.
Alisema
kinachotakiwa kwa wachezaji wake ni kujituma na kuanza vyema michuano hiyo.
Kocha
Selemani Matola alisema Yanga ni timu kubwa na nzuri hivyo anaamini mchezo utakuwa mgumu kwani mapungufu ya Yanga na mazuri ameyaona katika mchezo wa Ngao ya Jamii
Alisema
wamefanya maandalizi ya kutosha watahakikisha wanapambana na kupata pointi
tatu ugenini
No comments:
Post a Comment