Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, December 8, 2015

VAN GAAL AENDA GERMANY NA WACHEZAJI 19 ROONEY ABAKI NYUMBANI NA KUSHUHUDIA EVERTON

MENEJA wa Manchester United Louis van Gaal Leo amesafiri kwenda Germany na Wachezaji 19 kwa ajili ya Mechi yao ya mwisho ya Kundi B la UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, ambayo itaamua kama watasonga Raundi ya Mtoano au watatupwa EUROPA LIGI.
Man United hawawezi kutupwa nje kabisa ya Ulaya kwani matokeo ya aina yeyote ama yatwabakisha UCL au kupelekwa EUROPA LIGI wakimaliza katika Nafasi ya 3 ya Kundi B.
Katika Kikosi hicho cha Wachezaji 19 hayupo Kepteni Wayne Rooney na Kiungo Morgan Schneiderlin ambao ni Majeruhi na wanaungana na Majeruhi wengine Marcos Rojo, Ander Herrera, Phil Jones, Luke Shaw na Antonio Valencia.

UEFA CHAMPIONS LIGI
KUNDI: B:

PSV Eindhoven (Pointi 7) v CSKA Moskva (4)
Wolfsburg (9) v Manchester United (8)
-Wolfsburg watafuzu wakipata Sare na watachukua Nafasi ya Kwanza wakishinda.
-Man United watasonga wakishinda na kuwa Washindi wa Kundi.
-PSV watafuzu wakishinda au wakidroo ikiwa Man United itafungwa
-CSKA watatwaa Nafasi ya 3 wakiifunga PSV.
Miongoni mwa Kikosi hicho wapo Chipukizi kadhaa akiwemo Paddy McNair ambae alitolewa Haftaimu kwenye Droo na West Ham Majuzi na nafasi yake kuchukuliwa na Chipukizi wa Uruguay Guillermo Varela ambae nae yupo safarini.

Chipukizi wengine Kikosini ni Nick Powell, ambae muda mrefu hajajumuika katika Kikosi cha Kwanza na pia wapo Kiungo Sean Goss na Beki Cameron Borthwick-Jackson.

Kikosi kamili: David De Gea, Sergio Romero; Paddy McNair, Chris Smalling, Guillermo Varela, Cameron Borthwick-Jackson, Daley Blind, Matteo Darmian; Bastian Schweinsteiger, Michael Carrick, Sean Goss, Nick Powell, Ashley Young, Jesse Lingard, Andreas Pereira, Juan Mata; Memphis Depay, Marouane Fellaini, Anthony Martial.

Memphis Depay kwenye mazoezi huko Volkswagen Arena akijiweka tayari kupambana leo hii usku kwenye hatua ya mwisho

Van Gaal akiwacheki Vijana wake kwenye mazoezi kujiweka sawa dhidi ya Wolfsburg