Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 11, 2015

NAPE NNAUYE MGENI RASMI TUNZO YA MSANII 
WAZIRI wa Habari, Wasanii, Utamaduni, Vijana na Michezo, Nape Nnauye kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tunzo za Siku Ya Msanii zitakazofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho, Posta, Dar es Salaam.

Hii ni mara ya pili kwa tuzo za Siku Ya Msanii kufanyika, ambapo mara ya kwanza zilifanyika mwaka jana kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es  Salaam. Mwaka huu zitatolewa tunzo nne ikiwa ni nyongeza ya tunzo mbili  tofauti za zile za mwaka jana. Mwaka huu zitatolewa tunzo kutoka katika sekta ya  filamu, muziki, sanaa za maonyesho na sanaa za ufundi.

Meneja Uhusiano wa Siku Ya Msanii, Peter Mwendapole amesema walipeleka maombi wizarani kuomba Waziri atakayekuwa na dhamana ya Sanaa awe mgeni kwenye tukio la kesho. “Kwa hiyo kimsingi baada ya kuapishwa jioni Waziri Nnauye atakuwa kwenye hafla hii na wasanii nao watampa mahitaji yao na yeye akitoa mtazamo wa wizara kuhusu Sanaa na yeye pengine kuyatolea majibu”, alisema Mwendapole

 Mwendapole alisema katika burudani kutakuwa Mwanamuziki maarufu Richard Mangustino akiwa na bendi yake ya K-Mondo Muzika, kikundi cha Sanaa cha Safi, Mpuliza Saxaphone  Mafumu Bilal ‘Bombenga’ lakini pia wacheza sarakasi na yoga.Awali bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ watakuwa wanatoa burudani kwenye maonyesho ambao wao watakuwa kwenye burudani za awali sambamba na bendi ya Ifakara Sound kutoka, Ifaraka Morogoro.

Mwaka huu Tuzo hizo, zilianza na maonyesho ya kazi za wasanii ambapo wasanii kutoka mashirikisho manne ya sanaa walionyesha kazi zao katika viwanja vya makumbusho, Dar es Salaam.Mwaka jana washindi wa tuzo za Siku Ya Msanii walikuwa Father Canute Mzuwanda aliyeshinda tuzo ya Humanitarian wakati Said Tingatinga alishinda tuzo ya Life Time Achievement.

Siku Ya Msanii inaandaliwa na Haak Neel Production kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kudhaminiwa na New Habari (2006) LTD kupitia magazeti ya Bingwa, Dimba, Mtanzania na The African. Wadhamini wengine ni  Channel Ten, Magic FM na CXC, Kilimanjaro Twist.