Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 10, 2015

FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU KUANZA LEO JAPAN

KOMBE LA DUNIA kwa Klabu linaanza Japan leo. Washiriki wa Mashindano haya ni Barcelona, Mabingwa wa Ulaya, River Plate, Mabingwa wa Marekani ya Kusini, America ambao ni Mabingwa wa Nchi za Marekani ya Kati na Kaskazini na Visiwa vya Carribean, Mabingwa wa Afrika TP Mazembe, Guangzhou Evergrande, Mabingwa wa Asia na Bingwa wa Kanda ya Oceania.
Pia wapo Sanfrecce Hiroshima, Klabu Bingwa ya Japan, inayoshiriki kama Wenyeji wa Mashindano.
Wakati Barcelona wakiwa ndio wanategemewa kutwaa Kombe hili wakijivunia Kikosi chenye Masupasta Lionel Messi wa Argentina, Nahodha wa Brazil Neymar na Straika wa Uruguay Luis Suarez, Tanzania itaikodolea macho TP Mazembe yenye Mastraika Wawili mahiri kutoka Nchi hiyo, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Mwaka 2010, TP Mazembe ilifika Fainali ya michuano hii na kufungwa na Inter Milan.

Klabu ya China, Guangzhou Evergrande, pia itakodolewa macho kwa vile Kocha wao ni Mbrazil Luiz Felipe Scolari ambae aliisaidia kutwaa Ubingwa wa Asia.
Mechi ya ufunguzi ya Alhamisi ni kati ya Wenyeji Sanfrecce Hiroshima ikicheza na Auckland City katika Raundi ya Awali ambapo Mshindi atatinga Robo Fainali kucheza na TP Mazembe, inayoanzia hatua hii na Mechi hii itachezwa Jumapili huko Osaka.
Mshindi wa Robo Fainali hii atatinga Nusu Fainali kucheza na River Plate itakayoanzia hapo.
Katika Robo Fainali nyingine hapo Jumapili America itaivaa Guangzhou Evergrande na Mshindi wake kwenda Nusu Fainali kuikabili Barcelona itakayoanzia hapo.