Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, December 21, 2015

NANI KUIBUKA MSHINDI LEO, ARSENAL vs MANCHESTER CITY?

LEO JUMATATU Usiku ndani ya Emirates Jijini London ipo Mechi kubwa na muhimu kwa mustabali wa Ubingwa wa Ligi Kuu England Msimu huu wakati Arsenal na Manchester City zitakapokutana.
Ligi inaongozwa, bila kutarajiwa, na Leicester City ambao wako Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili Arsenal na Pointi 6 mbele ya Timu ya 3 Man City.
Hali hiyo inafanya Mechi hii kuwa muhimu mno kwa nani atamkaribia na kumkimbiza Leicester City wakati Ligi ikibakisha Mechi 2 kufikia nusu ya Msimu huu wa 2015/16.
Umuhimu wa Mechi unakuja pia kuona Wapinzani wengine wa jadi katika mbio za Ubingwa, Mabingwa Watetezi Chelsea na Man United, wakitetereka kwa Chelsea kuwa Nafasi ya 15 wakiwa Pointi 20 nyuma ya Leicester na Man United kushuka hadi Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 9 nyuma ya Vinara hao.
Kwa Arsenal, ushindi kwao dhidi ya City kutaleta matumaini kwao na Meneja wao Arsene Wenger ya kutwaa Ubingwa wa England ambao hawajauchukua kwa Miaka 12 sasa.
Lakini Timu zote hizi mbili wakati mwingine zimekuwa hazitabiriki hasa baada ya Mwezi uliopita Arsenal kupoteza Pointi 5 walipocheza na West Brom na Norwich City huku City wakipigwa pasipo kutarajia, ikiwemo 2-0 Mwezi uliopita dhidi ya Stoke City.