Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 4, 2015

NANI KUIBUKA KIDEDEA FAINALI ZA CECAFA CHALENJI CUP 2015 UGANDA NA RWANDA?


Rwanda na Uganda zimefanikiwa kuingia Fainali ya Kombe la Chalenji baada ya kushinda Mechi zao za Nusu Fainali kwa Mikwaju ya Penati.Katika Nusu Fainali ya kwanza, Sudan, waliocheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 23 baada ya Bakri Almadina kupewa Kadi Nyekundu, na Rwanda zilitoka 0-0 katika Dakika 90 na Gemu kwenda Nyongeza za Dakika 30 na ndipo Sudan kutangulia kufunga kwa Bao la Atahir Babakir la Dakika ya 100 lakini Rwanda walisawazisha kupitia Jean Baptiste Mugiraneza kwenye Dakika ya 110.
Rwanda walibaki Mtu 10 katika Dakika ya 121 baada ya Isaie Songa kupewa Kadi Nyekundu kwa kumpiga Kipepsi Beki wa Sudan.
Hadi Dakika za Nyongeza 30 kumalizika, Bao zilikuwa 1-1 na ndipo ikaja Mikwaju ya Penati Tano Tano ambazo Rwanda walitoka kidedea kwa Penati 4-2.
Nao Uganda na Wenyeji Ethiopia walicheza Dakika 120 bila kufungana na kisha Uganda kuingia Fainali kwa Penati 5-3.

RATIBA/MATOKEO:
Robo Fainali

Jumatatu Novemba 30

Uganda 2 v Malawi 0
Kilimanjaro Stars 1 v Sudan 1 [Ethiopia yasonga kwa Penati 4-3]

Jumanne Desemba 1
South Sudan 0 v Sudan 0 [Sudan yasonga kwa Penati 5-3]
Rwanda 0 v Kenya 0 [Rwanda yasonga kwa Penati 5-3]

Nusu Fainali
Alhamisi Desemba 3

Sudan 1 v Rwanda 1 [Sudan yasonga kwa Penati 4-2]

Uganda 0 v Ethiopia 0 [Uganda yasonga kwa Penati 5-3]

Jumamosi Desemba 5
Mshindi wa Tatu

Ethiopia v Sudan

Fainali
Uganda v Rwanda

No comments:

Post a Comment