Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, December 21, 2015

LOUIS VAN GAAL APEWA MECHI MOJA TU, AKIFUNGWA KUFUKUZWA


Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema anahofia kuhusu kazi yake na tayari kaambiwa ana Mechi Moja tu akichemsha anaondoka.
Juzi, kwa mara ya kwanza Msimu huu Uwanjani kwao Old Trafford, Man United walifungwa 2-1 na Norwich City na kuporomoka hadi Nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England. Jicho la kufukuzwa halijifichi!!! Jose (kulia) wakati akiutazama mchezo wa Championship kati ya Brighton na Middlesbrough.

Bao  zilifungwa na Cameron Jerome na Alex Tettey kwa Norwich wakati Anthony Martial akiifungia Man United kwenye Mechi ambayo Man United walitawala Mpira kwa Asilimia 75 lakini walipiga Shuti 2 tu Golini.
Matokeo hayo sasa yaliwafanya Man United wasiwe na ushindi katika Mechi 6 zilizopita na kufungwa Mechi 3 mfululizo.
Alipoulizwa kama anahofia kuhusu kazi yake, hasa baada ya Juzi Chelsea kumfukuza Jose Mourinho ambae ilidhaniwa hagusiki, Van Gaal alijibu: “Ndio, lazima uwe na wasiwasi!”
Pia, Van Gaal, mwenye Miaka 64, alishindwa kusema kwa uhakika kama Man United itampa muda zaidi kurekebisha mambo.

Alijibu: “Nadhani nitapewa lakini huwezi kujua kwa Dunia hii ya sasa. Si uamuzi wangu lakini tutaona.”
Mkataba wa Van Gaal na Man United unamalizika mwisho mwa Msimu ujao, ule wa 2016/17, na zipo habari za vyanzo thabiti kuwa Jose Mourinho ndie atakuwa Meneja mpya wa Man United endapo Van Gaal atatimuliwa.
Mourinho aliibuka na kusema anataka kurudia kazi yake haraka iwezekanavyo na kisha kuonekana kwenye Mechi ya Ligi Daraja la Championship kati ya Brighton na Middlesbrough.

Mechi zinazofuata kwa Man United kuelekea Krismasi na Mwaka Mpya ni dhidi ya Stoke City huko Britannia Stadium hapo Desemba 26, kisha Desemba 28 ni Old Trafford na Chelsea na kufuatia Swansea City Januari 2.