Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 21, 2015

MESSI NA RONALDO KUANZIA BENCHI LEO

HII ni El Clasico ya kwanza Msimu huu na inafanyika Jumamosi huko Santiago Bernabeu Jijini Madrid kati ya Wenyeji Real Madrid na Mabingwa Watetezi Barcelona katika Mechi ya La Liga.
Hii si Mechi itakayoamua Ubingwa lakini muhimu mno hasa kwa Real ambao wako Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 3 nyuma ya Vinara Barcelona.
Real, ambao walikuwa wakiongoza La Liga, waliteleza kwenye Mechi yao ya mwisho ya Ligi Wiki 2 zilizopita kabla Ligi haijasimama kupisha Mechi za Kimataifa, walipofungwa 3-2 na Sevilla.
Kitu ambacho kinangojewa kwa hamu ni kutaka kujua kama Kocha wa Barca, Luis Enrique, atamwanzisha Lionel Messi kwenye hii Mechi baada ya Mchezaji huyo kutocheza Mechi kwa Siku 54 akiuguza Goti lake.
Hata hivyo kukosekana kwa Messi hakukuizamisha Barca kwani Suarez na Neymar walipiga Bao zote 17 kwenye La Liga na kuwapaisha hadi kileleni.
Wachambuzi wanahisi Messi ataanzia Benchi la Barca ambayo pia itamkosa Majeruhi Rafinha huku Ivan Rakitic akiwa kwenye hati hati kama atacheza kutokana na maumivu.
Kwa Real, habari nzuri kwao ni kuwa Mastaa wao Gareth Bale na Cristiano Ronaldo hawakujiunga na Timu zao za Taifa kwenye hizo Wiki 2 za Mechi za Kimataifa na hivyo walibaki Bernabeu kujifua pamoja na Benzema, ambae alikuwa majeruhi lakini sasa yuko fiti, pamoja na Kepteni wao Sergio Ramos, aliahirisha operesheni ya Bega lake ili acheze.
Ramos atacheza hii El Clasico kwa msaada wa Sindano za kuzuia maumivu.
Mchambuzi mahiri huko Spain ametabiri kuwa Real itacheza Mechi hii ikitumia Mfumo wa 4-4-2 ambapo Bale na Ronaldo watakuwa Washambuliaji na Kiungo watasimama Isco, Kroos, Casemiro na Modric.

Kuhusu Barca, Mchambuzi huyo amedokeza kuwa Timu hiyo ilipokuwa haina Messi imetumia Mifumo tofauti, ile ya 4-2-3-1 na 4-4-2, lakini kwenye hii El Clasico Mfumo wao utategemea pia ikiwa kama Ivan Rakitic atakuwa fiti kucheza.
Hata hivyo, kawaida Barca hutumia Mafowadi Watatu na hii inamaanisha Munir El Haddadi anaweza kucheza pamoja na Suarez na Neymar.
Kwa upande wa Difensi, Mascherano anarejea baada ya kumaliza Kifungo na anatarajiwa kucheza Sentahafu pacha pamoja na Pique huku Busquets, aliekuwa akichezeshwa na Pique, kwenda nafasi yake ya kawaida ya Kiungo.
Golini, Barca watamsimamisha Claudio Bravo.

No comments:

Post a Comment