Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu
24 za makundi A, B, C na D kucheza katika viwanja 12 mbalimbali
nchini, kusaka nafasi nne za kupanda Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao
(StarTime First League).
Kesho Jumamosi Kundi A, Mvuvuma FC watakua wenyeji wa Abajalo FC ya
Tabora uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Transit Camp watacheza
dhidi ya Mirambo FC uwanja wa Kamabarage Shinyanga, huku Singida United
watawakaribisha Green Warriors katika uwanja wa Namfua mjini Singida.
Kundi B, Allicane FC watawakaribisha AFC ya Arusha uwanja wa CCM
Kirumba, JKT Rwamkoma watacheza dhidi ya Madini FC uwanja wa Karume
Musoma, Kundi C, Changanyikeni dhidi ya Karikoo ya Lindi watacheza
katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Mechi hizo zitaendelea kwa Kundi D, ambapo African Wanderes
watawakaribisha Sabasaba FC uwanja wa Wambi, Mafinga, Mkamba Rangers
dhidi ya Mbeya Warriors uwanja wa CCM Mkamba, na Wenda FC watacheza
dhidi ya Mighty Elephant uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa michezo mitatu kuchezwa
katika kundi B, na C, Pamba FC watawakaribisha Bulyanhulu FC uwanja wa
CCM Kirumba, Mshikamo dhidi ya Abajalo uwanja wa Mabatini, Mlandizi na
Villa Squad kuchuana dhidi ya Comsopolitan uwanja wa Karume jijini Dar
es salaam.
No comments:
Post a Comment