Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, October 20, 2015

RAUNDI YA 11 VODACOM KUCHEZWA DESEMBA 12 NA DARAJA LA PILI KUANZA NOVEMBA

BODI ya Ligi imepangua ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Akizungumza na wandishi wa habari jana Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Baraka Kizuguto alisema Mechi za raundi ya 11 za Ligi Kuu ya Vodacom zilizokuwa zichezwe Novemba 7 na 8 mwaka huu sasa zitafanyika Desemba 12 na 13 kupisha maandalizi ya Taifa Stars ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia.

“Taifa Stars inatarajia kuingia kambini mapema mwezi ujao kujiandaa na mechi ya kwanza dhidi ya Algeria ambayo itafanyika Novemba 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na zitarudiana nchini Algeria, Novemba 17 mwaka huu”,alisema Kizuguto.

Mechi hizo za Vodacom zitakazochezwa Desemba 12 ni kati ya Mgambo Shooting na Yanga utakaochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, Kagera Sugar na Ndanda kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Tabora, Stand United na Mwadui utakaochezwa Uwanja wa Kambarage Shinyanga.

Michezo mingine ni Mbeya City na Mtibwa Sugar utakaochezwa Uwanja was Sokoine Mbeya, Azam na Simba utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na Majimaji na Toto Africans utakaochezwa kwenye Uwanja wa Majimaji Songea. 

Mechi za Desemba 13 ni kati ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons utakaochezwa kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam, na Coastal Union na African Sports utakaochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Pia mechi tatu za raundi ya sita ambazo hazikuchezwa Oktoba 4 mwaka huu kupisha mechi ya Taifa Stars dhidi ya Malawi sasa zitachezwa Desemba 16 mwaka huu.
Mechi hizo ni Azam na Mtibwa Sugar utakaochezwa Uwanja wa Azam Dar es Salaam, na African Sports na Yanga utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga na  mchezo kati ya Ndanda na Simba kwenye Uwanja wa Nang’wanda Sijaona Mtwara utapangiwa tarehe ya kuchezwa.

Nayo mechi namba 59 kati ya JKT Ruvu na Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Oktoba 21 kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam imesogezwa mbele kwa siku moja hadi Oktoba 22 ili kuipa nafasi ya mapumziko JKT Ruvu ambayo jana (Oktoba 18 mwaka huu) ilicheza mechi yake ya raundi saba mkoani Shinyanga

 Pia Ligi Daraja la pili nchini (SDL) sasa itaanza Novemba 14 badala ya Oktoba 31 ili kutoa fursa kwa bodi ya Ligi kukamilisha maandalizi mengine ikiwemo viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michezo ya ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment