Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, October 20, 2015

RATIBA - UEFA CHAMPIONS LEAGUE NI ARSENAL vs BAYERN MUNICH

Arsenal hawana njia yoyote ila kuwashambulia Bayern Munich Uwanjani Emirates Jumanne Usiku kwenye Mechi ya Kundi F la UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, kwa mujibu wa Meneja wao Arsene Wenger.

Arsenal wamechapwa Mechi zao zote mbili za Kundi F kutoka kwa Dinamo Zagreb na Olympiakos na wapo mkiani mwa Kundi hilo na Mechi zao 2 zinazofuata ni dhidi ya Mabingwa wa Germany Bayern Munich.Ikiwa Arsenal watafungwa na Bayern basi wapo hatarini ya kutofuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL kwa mara ya kwanza katika Miaka 16.
Hii si Mechi rahisi kwa Arsenal kwani Bayern watatinga Jijini London Uwanjani Emirates wakiwa na wimbi la ushindi la Mechi 12 mfululizo.

Lakini hilo halimtishi Wenger ambae amesema: “Sasa tupo katika hali nzuri na mkazo kwetu ni Mechi hii ya Jumanne.”
Arsenal hivi sasa wapo kwenye wimbi zuri la ushindi kwenye Ligi Kuu England ambalo limewapaisha hadi Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 tu nyuma ya Vinara Man City.

Mara ya mwisho kwa Arsenal na Bayern kukutana kwenye UCL ni Mwaka Jana walipotoka 1-1 huko Allianz Arena Jijini Munich na Bayern kushinda 2-0 Uwanjani Emirates katika Mechi yao ya kwanza.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE
MAKUNDI
Jumanne Oktoba 20
KUNDI E

BATE Borislov v Barcelona
Bayer Leverkusen v AS Roma

KUNDI F
Arsenal v Bayern Munich
Dinamo Zagreb v Olympiakos

KUNDI G
Dynamo Kiev v Chelsea
FC Porto v Maccabi Tel Aviv

KUNDI H
Valencia v KAA Gent
Zenit Saint Petersburg v Lyon

Jumatano Oktoba 21
KUNDI A

Malmö FF v Shakhtar Donetsk
Paris St Germaine v Real Madrid

KUNDI B

CSKA v Man United
VfL Wolfsburg v PSV

KUNDI C

Atletico Madrid v FC Astana
Galatasaray v Benfica

KUNDI D

Juventus v Borussia Mönchengladbach 

Man City v Sevilla

No comments:

Post a Comment