STRAIKA wa Chelsea Diego Costa
a,mieiambia BBC katika Kipindi cha Football Focus kwamba anajijuja yeye
‘si Malaika’ akiwa Uwanjani lakini hatabadili tabia yake ya upiganaji.
Msimu huu, Costa ameshafungiwa Mechi 3
mara mbili kwa kumtimba Mchezaji wa Liverpool Emre Can na kisha
kukwaruzana na Laurent Koscielny wa Arsenal.
Costa, Mzaliwa wa Brazil mwenye Miaka
27, amesema yeye amefika hapo alipo kwa kucheza hivyo hivyo na
habadilika kwa sababu Watu wanataka tu. Costa alihamia Chelsea Julai 2014 na kuisadia kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England na Capital One Cup Msimu uliopita.
Mameneja kadhaa wa Timu pinzani huko England wameshajitokeza kumlaumu kwa kuwa mkorofi, mchokozi na mgomvi Uwanjani huku Meneja wa Man City, Manuel Pellegrini, akimtaka apunguze tabia yake wakati Arsene Wenger wa Arsenal akimlaumu sana kwa kuwa mchokozi mkubwa.
Hata Meneja wa Timu ya Taifa ya Spain ambayo Costa huchezea, Vicente del Bosque, amelaumu matendo yake ya hivi karibuni.
Lakini mwenyewe Costa amepinga na kusema Soka si lele mama na yeye hachezi legelege.
Msimu uliopita, Costa alifunga Bao 20 kwa Chelsea lakini Msimu huu ana Bao 3 tu hadi sasa wakati Chelsea wakiselelea Nafasi ya 12 kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Man City.
Jumamosi kwenye Ligi Kuu England, Chelsea wanapambana West Ham ambayo ipo Nafasi ya 3.
No comments:
Post a Comment