NAHODHA wa Tanzania Prisons, Laurian Mpalile amesema mchezo dhidi
ya Mbeya City utakuwa mgumu lakini haiwafanyi
kuogopa kucheza nao.
Mpalile alisema hasira za
kufungwa na Yanga wanakwenda kuzimalizia kwa Mbeya City japo wanafahamu ni timu
nzuri na inafundishwa na mwalimu mzuri.
“Tumefungwa na Azam FC mabao 2-1,
jana (juzi) tumefungwa na Yanga wametufunga mabao 3-0, ni matokeo mabaya kwetu
hivyo hasira zetu tutazimalizia kwa Mbeya City japo tunapokutana nao mchezo
huwa mgumu”, alisema Mpalile
Pia Mpalile alisema dakika 20 za mwanzo walicheza kwa kuzuia zaidi huku wakitumia nguvu
kutokana na maelekezo ya kocha kuona Yanga wanafanya mashambulizi yao kupitia
wapi na kusahau kwenda kunashambulia.
Mpalile alimtupia
lawama golikipa wao na kusema mabao mawili ya mwanzo
walifungwa kutokana na makosa yake lakini wanamheshimu kwa sababu ni makosa ya
mchezo ambayo hata mchezaji mwingine anaweza kufanya.
Pia nahodha huyo
amekiri kadi nyekundu aliyooneshwa beki wao Josephat ilikuwa sahihi kwa sababu alikuwa
ni mchezaji wa mwisho alipomfanyia Msuva rafu ya nyuma ‘tackling from behind’ akiwa
ndani ya eneo la goli
Mpalile pia alisema kubadilisha makocha kwenye timu inachangia
yetu kufanya vibaya kwasababu kila kocha anakuja na falsafa yake hivyo inakuwa
vigumu kubadilika haraka kuendana na matakwa ya kocha.
No comments:
Post a Comment