Kituo cha Mazoezi cha Home Gym…
Na Andrew Chale, modewjiblog
[Dar
es Salaam-Tanzania]- Kuelekea miaka 17 ya tangu kuanzishwa kwa kituo
cha Mazoezi cha Home Gym chenye maskani yake Mwenge jijini Dar es
Salaam-Tanzania, uongozi wa kituo hicho unatarajia kufanya matukio makuu
muhimu ikiwemo kutembelea wodi ya akina mama katika kituo cha Afrya
cha Sinza Palestina Jijini.
Akizungumza
na modewjiblog, Mkurugenzi wa kituo hicho, Andrew Mangomango
amebainisha kuwa, kuelekea shughuli za miaka 17 za tangu kuanzishwa
kwake kituo hicho, hiyo Septemba 20, siku moja kabla yaani leo
Septemba 19, watafanya tukio la kufariji wagonja kwenye kituo cha afya
cha Sinza Palestina ambapo pia watatoa zawadi mbalimbali kwa walengwa
akina mama pamoja na zoezi la ufanyaji usafi.
“Septemba
19, uongozi wa wadau wote tutatembelea kituo cha Afya cha Sinza
Palestina na kufariji wagonja katika wodi ya wazazi. Hii ni pamoja na
kutoa vitu muhimu vinavyowakabili wazazi hasa katika masuala mazima ya
uzazi.” Amesema Andrew Mangomango.
Mkurugenzi
huyo ameongeza kuwa, kutokana na mazoezi ni afya, hivyo wataendelea
kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuakikisha wanasaidia afya za
watu wote hapa nchini ikiwemo kuimalisha miili yao kupitia mazoezi
mbalimbali hasa ya viungo.
Aidha,
katika upande wa shughuli ya Septemba 20 yaani kesho, ambayo watakuwa
wakisheherekea miaka hyo 17, tangu kuanzishwa kwa Home gym,
wanatarajia watu zaidi ya 500, kushiriki katika Bonanza hilo.
Zoezi
hilo linataraiwa kuhusisha vikundi mbalimbali vya jogging, vituo vya
gym mbalimbali siku ya juma pili hii ya septemba 20 katika viwanja vya
Escape One.
Andrew
Mangomango anabainisha kuwa, zoezi hilo litaanzia Mlimani City majira
ya saa kumi na mbili asubuhi kwa washiriki kukimbia kwa mwendo wa
taratibu pamoja na kutembea kwa makundi na kuishia viwanja vya Escape
One.
Ratiba ya Bonanza:
Baada
ya kuwasili katika viwanja vya Escape One, saa mbili asubuhi itaanza
AEROBICS mpaka saa nne asubuhi na mara baada ya hapo kutakuwa na michezo
mbalimbali ikiwemo kuvuta Kamba, kukimbia na magunia, kukimbiza kuku
kunyanyua vitu vizito , kutunisha misuli, mpira wa miguu pamoja na
Burudani ya muziki, lakini pia kutakuwa na michezo mbalimbali kwa
watoto hivyo kuwataka wazazi kwenda na watoto wao ili kufurahia kwa
pamoja.
Bonanza
hilo limebeba kauli mbiu isemayo FANYA MAZOEZI KWA AFYA YAKO likiwa na
lengo la kuwahamasisha watu wote kushiriki katika mazoezi ili kutunza
afya zao.
Kituo
hicho cha mazoezi kilichoanzishwa mwaka 1998 kimekuwa na mchango
mkubwa katika kujenga na kulinda afya za watu wengi kupitia mazoezi
mbalimbali yanayotolewa kwenye kituo hicho kwa kipindi chote.
Moja ya matukio ya Bonanza la mazoezi la kityuo hicho cha Home Gym (picha kwa hisani ya gazeti la Mwananchi)
Baadhi
ya vifaa vya kisasa kabisa vya mazoezi katika kuimalisha mwili ambapo
Home gym wanayatoa pia kwa watu mbalimbali kwenye kituo chao hicho cha
mazoezi, Mwenge jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment