PAMOJA na kuanza vema ligi huku akiwa
amefunga mabao mawili, Hamis Kiiza amesema hawezi kusema hayo ni mafanikio.
Kiiza ambaye anachezea Simba msimu huu baada
ya Yanga kumwacha msimu uliopita amefanikiwa kufunga mabao mawili kwenye uwanja
wa Mkwakwani jambo linalotafisiriwa kuwa Simba imevunja mwiko kwani ilizoeleka
kupoteza mechi kwenye uwanja huo.
“Nashukuru
timu imeanza vizuri kitu ambacho ni kizuri kwa sisi
wachezaji na wapenzi wa Simba lakini bado hatuwezi kusema haya ni mafanikio bado
tunataka kuendelea kufanya vizuri na tunapofanya vizuri kila kitu atafurahi”,
alisema Kiiza
Pia Kiiza alisema Simba kuna umoja kwani kwenye
timu kila mmoja anajituma na anajua umuhimu wa ushindi
Kiiza alisema kila timu wanayocheza nayo wanaiheshimu
kwani wanajua kila timu ni ngumu na wao wanakwenda kwa ugumu ili wapate matokeo
mazuri, kiujumla tunafanya vizuri kwasababu ya ‘team work’ tunapendana wote.
Pamoja
na kuanza vizuri
lakini ameshindwa kuahidi kuwa atafunga mabao mangapi ila alisema anataka kuisaidia
timu yake kufanya vizuri, kupata pointi tatu hata kama hajafunga anaweza
kutengeneza watu wakafunga wakapata ushindi lakini sio Kiiza kuibuka mfungaji
bora na timu haijachukua ubingwa.
Kiiza alisema timu ni
sehemu yake ya kazi na yeye anaheshimu kazi anapokuwa kazini na kusema
alivyokuwa Yanga, alikuwa anaipenda kazi yake ndio maana alifanikiwa na sasa
hivi yupo Simba anafanya vizuri anaipenda kazi yake ndio maana ametulia kwani
amekuja Tanzania kufanya kazi, hajaja kufanya mapenzi.
No comments:
Post a Comment