HATIMAYE Mume wa muimbaji
wa nyimbo za injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha (32) ameachiwa huru jana
katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, baada ya upande wa mshitaka kushindwa
kuthibitisha mashitaka ya kubaka yaliyokuwa yanamkabili.
Baada ya kuachiwa huru,
Mbasha alitoka mahakamani hapo ambapo alipiga magoti na kulia huku amenyanyua mikono juu ishara ya
kumshukuru Mungu.
Akisoma hukumu hiyo jana
kuanzia saa 4:45 hadi saa 5:15 asubuhi
asubuhi, Hakimu Mujaya alisema Mbasha alikabiliwa na mashitaka mawili ya kubaka.
Alisema kwamba mahakama
hiyo ilisikiliza mashahidi sita wa upande wa mashitaka akiwemo muhangwa wa
tukio hilo ambaye ni shemeji wa Mbasha mwenye umri wa miaka 17 na Flora.
Hukumu hiyo ambayo
ilisikilizwa katika chumba cha siri (chamber Court) Hakimu Mjaya alisema
shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, ambaye ni shemeji wa mbasha aliiambia
mahakama kuwa Mei 23 mwaka jana alibakwa na Mbasha nyumbani kwake, Tabata
Kimanga baada ya Flora kwenda kuchukua CD za nyimbo zake.
Pia alisema shahidi huyo
alidai alibakwa kwa mara ya pili katika gari aina ya Ipsum walipokuwa wanatoka
kumtafuta Flora ambaye alikuwa haonekani nyumbani.
Akipitia ushahidi wa Daktari
wa Hospitali ya Amana, Migole Mtuka, hakimu huyo alisema, daktari huyo alidai
ndiye alimfanyia vipimo msichana huyo na kuwa hakuona dalili zozote za
kuingiliwa kimwili na Mbasha.
Alisema daktari huyo alidai
kuwa binti huyo alifika hospitalini hapo Mei 26, mwaka jana, kwa ajili ya
kufanyiwa vipimo na baada ya kumtaka kwenda maabara, hakwenda bali alitoroka
na kurejea Juni 3, mwaka jana, baada siku nane kupita.
Hata hivyo, Hakimu Mjaya
alisema kupitia mashahidi wote mahakama iliona mapungufu katika ushahidi huo
ambapo ilimuona mshitakiwa hana hatia.
‘’Kupitia ushahidi huu
mahakama imebaki na maswali kama kweli umebaka au la. Kwa hivyo upande wa
mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka haya bila ya kuacha shaka na mahakama
inakuachia huru,’’ alisema Hakimu Mjaya.
Mbasha alifika mahakamani hapo akiongozana na mdogo
wake wa kiume pamoja na Wakili wake, Mathew Kakamba.
Akizungumza na waandishi wa
habari nje ya mahakama hiyo, Mbasha alisema Mungu ni mwema huku akifuta machozi
na kuwaambia waandishi kuwa watawasiliana.
Awali, Mbasha alifikishwa
kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Juni 17 mwaka jana akitokea Kituo cha Polisi
Tabata, Dar es Salaam na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Wilberforce
Luhwago.
Jalada la kesi hiyo
liliamishwa kwa Hakimu Mkazi, Flora Mujaya baada ya Hakimu Luhwago kuwa na
majukumu mengine ya kazi.
Katika kesi hiyo,
Mbasha alikabiliwa na mashitaka mawili ya ubakaji ambapo ilidaiwa alitenda
makosa hayo maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.
Katika mashitaka
ya kwanza ilidaiwa Mei 23, mwaka jana maeneo hayo, Wilaya ya Ilala, kinyume cha
sheria za nchi, alimbaka msichana huyo.
Pia ilidaiwa kuwa
Mei 25, mwaka jan, maeneo la Tabata Kimanga nyumbani kwa mshitakiwa alimbaka tena mlalamikaji huyo.
Hata hivyo, mshitakiwa
alikana mashitaka hayo na kuwa nje kwa dhamana
baada ya kulala siku moja katika mahabusu ya Keko.
Mwishooo
No comments:
Post a Comment