TIMU ya soka ya kiluvya United ‘Wabishi wa Pwani’ juzi
walianza vema kivumbi cha ligi daraja la kwanza baada ya kuichapa timu ya Ashanti united
ya Jijini Dar es salaama kwa mabao 2-0
katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa mabatini Mlandizi.
Mchezo huo wa ligi daraja la kwanza ulikuwa na ushindani
mkali kutokana na timu zote mbili kucheza mpira wa kasi katika dakika za
kipindi cha kwanza kwa lengo la kuweza kuondoka na ushindi na kujinyakulia
pointi tatu muhimu lakini hadi hadi
mapumziko hakuna mbambe aliweza kuzifumania nyavu za mwenzake.
Kipindi cha pili timu ya Kiluvia United ilionekana kuingia
kwa kubadilisha mfumo wa mashambulizi na kuanza kulisakama lango la wapinzani
wao na kufanikiwa kuandika bao la kwanza kunako katika dakika ya 47 lililowekwa
kimiani na mshsambuliji wao wa kutumaniniwa Chala Juma.
Kuingia kwa bao hilo kuliweza
kulionekana kuwachanganya wachezaji wa Ashanti United kwa kujipanga upya
na kujaribu kuongeza kasi zaidi kwa lengo la kupata bao la kusawazisha lakini
kutokana na safu ya ulinzi ya Kiluvya United kuwa imara waliweza kuthibiti
mashambulizi ya wapinzani wao.
Mchezaji Kulwa Muanda pamoja na kimo chake kuwa ni kifupi
aliweza kuonyesha uwezo wake katika kulisakata kabumbu baada ya kuwainua
mashambiki wa kiluvva united baada ya kupachika bao la pili baada ya
kuiunganisha krosi safi iliyochongwa Chala Juma
na kuwamwacha mlinda mlango wa Ashanti United amebaki mdomo wazi.
Ashanti United licha ya kuwahi kuonja joto la kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara
walijikuta wanakabwa koo na wabishi hao wa Pwani na kupelekea hadi kipenga cha
dakika tisini kinapulizwa timu ya Kilivya ilitoka uwanjani hapo kifua mbele kwa
ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzania wao.
Mara baada ya kumalizika kwa matanange huo mlezi wa timu
hiyo Edward Mgogo almaarufu (Eddo Master) alisema kwamba vijana wake wameonyesha mchezo mzuri na kupatikana na
ushindi huo ni kutokana na kujituma katika dakika zote za mchezo huo.
Aidha Eddo alisema
kwamba ana imani vijana wake wataweza kufika mbali na kufanya vizuri katika
ligi daraja la kwanza na kuwaomba wadau wa Mkoa wa Pwani mchezo wa kandanda kwa ujumla sambamaba na wana kiluvya wote
kuhakikisha wanaipa ushirikiano wa dhati
timu hiyo katika ligi hiyo ya daraja la kwanza amabyo inaushindani mkubwa
kutokana na kuzishirikisha timu amabzo zilishawahi kushiriki ligi kuu ya
Tanzania bara.
No comments:
Post a Comment