Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, September 15, 2015

MANCHESTER UNITED WAIFUATA PSV EINDHOVEN KWAO BILA WAYNE ROONEY, MECHI KUCHEZWA USIKU, MARTIAL NA DEPAY KUANZA

Kikosi cha Wachezaji wa Man United wameonekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Manchester wakijiandaa kupaa kwa ndege kuelekea Eindhoven tayari kwa mchezo wao wa Uefa Champions Ligi.

Ndani ya kikosi hicho waliambatana na Vijana wao matata Anthony Martial na Memphis Depay ambao wameonekana katika Mchezo huo wenda wakaanzishwa kwa kile kilichoonekana kwamba hawakuambatana na Straika wao na Nahodha Wayne Rooney ambaye ana majeraha yaliyomfanya pia hakose mchezo wa jumamosi dhidi ya Liverpool.
David De Gea nae alikuwemo katika msafara huo, Mchezo huo utapigwa kesho jumanne saa 3:45 usiku kwa saa za hapa kwetu Tanzania. 

Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney ameachwa nje ya kikosi kitakachocheza mechi ya Ligi ya Kilabu Bingwa Ulaya Jumanne ugenini PSV Eindhoven kwa sababu ya jeraha.
Rooney, 29, hakucheza kwenye mechi yao dhidi ya Liverpool Jumamosi baada yake kuumia misuli ya paja akifanya mazoezi. Kilabu hiyo ya Old Trafford ilishinda 3-1 kwenye mechi hiyo.
Mkufunzi mkuu wa Red Devils Louis van Gaal alisema kulikuwa na shaka kuhusu mchezaji huyo baada ya mechi hiyo, na sasa amesema ameamua kutobahatisha.
Mshambuliaji James Wilson na kiungo wa kati Andreas Pereira wamejumuishwa kikosini.
Wawili hao hawajacheza mechi yoyote msimu huu, na majuzi Wilson alihusishwa na kuhamia kilabu inayocheza ligi ya daraja la pili kwa mkopo.
Pereira naye amechezea klabu hiyo mechi mbili pekee akiingia kama nguvu mpya, tangu ajiunge nao kutoka PSV Agosti mwaka jana.
Mechi hiyo ya Ligi ya Kilabu Bingwa Ulaya itakayochezwa Jumanne uwanja wa Phillips itakuwa ya kwanza kwa Manchester United kwenye kampeni yao Kundi B.
Meneja wa Man United Louis van Gaal aliwongoza Vijana wake kwenda  Eindhoven
Kipa David De Gea
Anthony Martial na Morgan Schneiderlin Marouanne Fellaini
Fellaini

Depay

Ashley Young

BlindJuan Mata and Marcos Rojo
Juan Mata na Marcos Rojo
Michael Carrick
Michael CarrickLuke Shaw, Smalling, Antonio  Valencia na FellainiKipa David De Gea

No comments:

Post a Comment