Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, August 5, 2015

NAHODHA WA FC PLATINUM THABANI KAMUSOKO ATUA KUZIBA NAFASI YA SHERMAN



 
Mchezaji mpya wa Yanga Mzimbabwe Thabani Kamusoko (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  jana. Kulia ni Meneja wa Hafidhi Saleh



HATIMAYE kiungo na nahodha wa FC Platinum ya Zimbabwe, Thabani  Michael Kamusoko ametua jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kusaini mkataba wa kujiunga na Yanga.

Kamusoko alipokewa na Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), ambapo alipelekwa katika kikao na uongozi kwa mazungumzo.

Akizungumza uwanjani hapo baada ya kutua mchezaji huyo, alisema amekuja kikazi zaidi na Yanga hawatajutia kumsajili endapo watafikia makubaliano.

Kamusako aliyewahi pia kuchezea Dynamos FC ya Zimbabwe, anatarajia kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Yanga.

Mchezaji huyo rasta aliyeivutia Yanga ilipokutana na FC Platinum katika Kombe la Shirikisho mwanzoni mwa mwaka huu, anatarajia kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mghana Kpah Sherman aliyeuzwa Mpumalanga Black Aces ya Afrika Kusini.

Lakini pia, Yanga iko mbioni kuwaacha wachezaji wake wengine wawili wa kigeni, beki Mghana Joseph Tetteh Zutah na kiungo Mbrazili Andrey Coutinho.

Dirisha la usajili Tanzania Bara linatarajiwa kufungwa saa 6:00 usiku leo huku ikibaki nafasi ya kuwasajili wachezaji huru pekee.

Baada ya Yanga kutolewa katika robo fainali michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, imekitathmini kikosi chake na kugundua Zuttah na Coutinho hawana faida.

Coutinho alijiunga na Yanga SC msimu uliopita akiletwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mbrazili mwenzake, Marcio Maximo na hadi sasa ameichezea timu hiyo mechi 33 na kuifungia mabao sita.

Mbrazili huyo alikuwa ana wakati mzuri chini ya kocha Maximo, lakini tangu ujio wa Mholanzi, Hans van der Pluijm hana namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Zuttah amesajiliwa Juni mwaka huu kutokana na kupendekezwa na kocha Pluijm, lakini baada ya wiki mbili za Kombe la Kagame, uongozi umeona hana umuhimu.

Mbali na Sherman, Coutinho na Zuttah, wachezaji wengine wa kigeni waliopo Yanga ni Mkongo Mbuyu Twite, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma.

Yanga SC ilifungwa kwa penalti 5-3 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika robo fainali ya Kagame dhidi ya Azam FC wiki iliyopita na tathmini ya baada ya mashindano, inaonesha timu inahitaji marekebisho kadhaa.



No comments:

Post a Comment