Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, July 30, 2015

WAAMUZI WA WATAKAOCHEZESHA LIGI KUU NA DARAJA LA KWANZA KUPIMWA AGOSTI 21-24



KOZI ya waamuzi wa mpira  wa miguu watakaochezesha mechi za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza 2015/2016, inatarajiwa kutafanyika jijini Dar es salaam kuanzia Agosti 21 -24.
Akizungumza na wandishi wa habari Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) , Baraka Kizuguto, alisema shirikisho  kozi  ya waamuzi watakaochezesha mechi za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2014/2015 wenye umri wa miaka 21 – 45 kwa wanawake na miaka 23 – 45 kwa wanaume. 
“Waamuzi wote wanatakiwa kuripoti Agosti 21 katika ofisi za TFF zilizopo Karume Ilala Dar es salaam na wawasilishe vyeti halisi vya kuzaliwa na nakala zake”, alisema Kizuguto
Pamoja na cheti cha kuzaliwa kwa kila mwamuzi ni lazima alete kadi ya kupigia kura au passport ya kusafiria kwa ajili ya uthibitisho wa umri wake.
Washiriki wa kozi watafanya mitihani ya kupima afya, utimamu wa mwili na sheria za mpira wa miguu Trivia (kuandika), mikanda ya video za sheria za soka na uchambuzi wa mechi.
Waamuzi watakaofaulu watashindanishwa kupata waamuzi 40 na waamuzi wasaidizi 70 watakaochezesha Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza kwa msimu wa 2015/2016. 
Baada ya kozi ya waamuzi kutakuwa na kozi ya makamisaa wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza ambayo itafanyika kuanzia Agosti 24-25 na wanatakiwa kuripoti Agosti 23saa 10:00 alasiri uwanja wa Taifa.
Makamisaa watafanya mtihani wa sheria za mpira wa miguu, na kupima mwamuzi anapochezesha  na wale watakaofaulu ndiyo watakaopangwa kusimamia michezo hiyo.


No comments:

Post a Comment