Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, July 14, 2015

MAGUFULI MGENI RASMI CECAFA JUMAMOSI

www.bukobasports.com

WAZIRI wa Ujenzi, John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa michuano ya Kombe la Kagame yanayofanyika nchini kuanzia Julai 18 2015 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Magufuli ambaye ameteuliwa kuwa mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi  (CCM) hivi karibuni baada ya kufungua rasmi michuano hiyo, atashuhudia mechi itakayokutanisha miamba ya Afrika Mashariki timu ya Yanga dhidi ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya.

Akizungumza na wandishi wa habari Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Baraka Kizuguto alisema kuwa taratibu zote zimekamiliki na timu zitaanza kuwasili kesho wakati waamuzi wanaanza kuwasili leo.

“Waamuzi wa michezo hiyo wanatarajiwa kuwasili kesho (leo) sambamba na kamati ya ufundi kwa ajili ya mitihani ya utimamu wa mwili (Physical Test) itakayofanyika siku ya alhamisi, na kamati ya ufundi watakua wakikagua viwanja na kuweka vipimo kabla ya ufunguzi rasmi wa michuano hiyo”, alisema Kizuguto

Michuano ya Kagame inatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya jumamosi kwa michezo mitatu, ukindoa mechi ya Yanga na Gor Mahia, mechi zingine zitakua ni kati ya APR dhidi ya Al Shandy uwanja wa Taifamchezo utakaochezwa  saa 8 mchana wakati KMKM na Telecom zitacheza uwanja wa Karume saa 10 jioni.

Yanga inayofundishwa na Hans van Pluijm imewahi kutwaa ubingwa mara tano (Mwaka 1975, 1993, 1999, 2011, na 2012) wa michuano hiyo watakuwa na kazi moja tu ya kujaribu kuifikia rekodi ya Simba, inayoongoza kutwaa Kombe hilo mara nyingi, ikiwa imeweza kufanya hivyo, mara sita. 

Pia Yanga imemaliza kama washindi wa pili mara mbili, mwaka 1976 ilipofungwa na Gor Mahia 2-1 jijini Kampala na mwaka 1992 ilipolala kwa mikwaju ya penati mbele ya watani wao wa jadi, Simba.

Gor Mahia ambayo inafunzwa na kocha Frank Nuttal, raia wa Uskochi mara ya mwisho kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1985, lakini imetwaa ubingwa huo mara 5 (1976, 1977, 1980, 1981, 1985) hivyo kama ilivyo Yanga wana kazi ya kuakikisha wanavunja rekodi ya Simba ambayo mwaka huu haishiriki.

Mchezo wa ufunguzi  kati ya Yanga dhidi ya Gor Mahia unaonekana kuteka hisia za wapenzi wa soka kwa ukanda wa Afrika Mashariki, kwani ni takribani miaka 19 timu hizo mbili haziwaji kukutana katika ardhi ya Tanzania.

 Gor Mahia na Yanga zipo kwenye kundi A pamoja na timu za Al Khartoum ya Sudan, KMKM ya Zanzibar na Telecom ya Djibout.

No comments:

Post a Comment