KOCHA wa
timu ya APR ya Rwanda, Dusan Dule Suyagic amejigamba
kuwa kikosi chake kitafanya vizuri kwenye mashindano ya Kagame inatarajiwa
kuanza kutimua kesho jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
baada ya mazoezi na timu yake yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dusan alisema msimu uliopita timu yake
ilishika nafasi ya pili baada ya kufungwa na El Merreikh ya Sudan hivyo msimu
huu wamekuja wakijua kuna ushindani lakini nao watahakikisha wanatoa ushindani.
“Naheshimu
kila timu iliyopo kwenye mashindano haya lakini naamini APR tutaonyesha
ushindani kwani lengo letu ni kutwaa ubingwa wa CECAFA”, alisema Dusan.
APR itafungua
dimba la mashindano ya Kagame ambayo yanashirikisha klabu toka nchi za Afrika
Mashariki na Kati kwa na Al Shandy ya Sudan kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja
wa Taifa saa 8 kabla ya Yanga na Gor Mahia kuingia dimbani saa 10.00 kumaliza
ubishi wa mashabiki kuwa nani mkali kati ya hizi timu kongwe Afrika Mashariki.
Mashindano ya CECAFA yanashirikisha vilabu 13 toka nchi za ukanda wa
Afrika Mashariki na Kati ambapo APR FC ipo kundi B pamoja na Al Shandy ya
Sudan, LLB AFC ya Burundi na Hegaan FC ya Somalia.
Kundi A lina timu za Yanga na KMKM za Tanzania, Telecom ya Djibout,
Gor-Mahia ya Kenya na Khartoum ya Sudan wakati kundi C lina timu za Azam ya Tanzania,
Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda.
No comments:
Post a Comment