Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 1, 2015

ARGENTINA YAICHAPA PARAGUAY 6 -1 KWENYE COPA AMERICA, FAINALI SASA NI USO KWA USO NA WENYEJI CHILE

Wachezaji wa Argentina wakipongezana baada ya kuifunga bao 6-1 ParaguayNdani ya Estadio Municipal Alcaldesa Ester Roa Mjini Rebolledo Nchini Chile, Argentina wameitandika  Paraguay katika Nusu Fainali ya Pili ya Copa America. BAO za  Argentina  zimefungwa na
Marcos Rojo 15'
Javier Pastore 27'
Ángel Di María 47' 
Ángel Di María 53 

Bao la Paraguay limefungwa na Lucas Barrios dakika ya 43 kipindi cha kwanza.
Ushindi wa Argentina asubuhi hii kuifanya kwenda nusu Fainali na kukutana uso kwa uso na Wenyeji Chile ambao wametinga Fainali baada ya kuichapa Peru 2-1.Lionel Messi
Baada ya kukutana awali katika Mashindano haya na kutoka Sare 2-2 katika Mechi ya Kundi lao ambayo Argentina waliongoza Bao 2-0 kabla Haftaimu na Paraguay kusawazisha, safari hii pia Argentina waliongoza 2-0 kwa Bao za Marcos Rojo na Pastore, zilizotengenezwa na Nahodha wao Lionel Messi.

Lakini safari hii kulikuwa hamna kufufuka kwa Paraguay kwani walipata pigo kubwa baada ya Mastraika wao wote Wawili, Derliz Gonzalez na Roque Santa Cruz, kuumia na kutolewa.
Lucas Barrios, alieingia kuchukua moja ya nafasi hizo, alifufua matumaini kwa Paraguay alipofunga Bao na Timu kwenda Mapumziko Gemu ikiwa 2-1.
Lakini Kipindi cha Pili, Bao za Angel Si Maria, Bao 2, Sergio Aguero na Gonzalo Higuian, alieanzia Benchi, ziliwapa Argentina ushindi wa Bao 6-1.

No comments:

Post a Comment