Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 1, 2015

KIIZA WA YANGA KUJIUNGA NA SIMBA ENDAPO ATAFUZU VIPIMO VYA AFYA



UONGOZI wa Simba umesema mchezaji wa zamani wa Yanga Hamis Kiiza atajiunga na klabu hiyo kwenye mazoezi kati ya leo au kesho iwapo tu atafuzu vipimo vya afya.

Kiiza ambaye alitemwa Yanga msimu uliopita alitarajiwa kuwasili wakati wowote kuanzia jana, na leo atapimwa afya ili kuungana na wachezaji wengine wa Simba katika mazoezi.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari leo  Rais wa Simba Evans Aveva alisema Kiiza atakuwa mchezaji halali wa Simba iwapo atafuzu vipimo leo.

“Kiiza atatua muda wowote kuanzia leo na akifaulu vipimo vya afya moja kwa moja atakuwa mchezaji wetu,”alisema.
Mchezaji huyo Mganda alitemwa na aliyekuwa Kocha wa Yanga Marcio Maximo msimu uliopita na nafasi yake kuchukuliwa na Kpah.

Kiiza hivi karibuni alinukuliwa kwenye vyombo vya habari akithibitisha ujio wake wa kujiunga na Simba.

Iwapo atafanikiwa kusajiliwa Simba atatimiza jumla ya wachezaji wanne  wanaotoka Uganda baada ya Emmanuel Okwi na Simon Sserunkuma na Juuko Murshid huku Raphael  Kiongera akitokea Kenya.

No comments:

Post a Comment