Ramadhan Singano akiongea na wandishi leo |
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetumia busara kumaliza
sakata la mkataba wa mchezaji wa Simba Ramadhan Singano na uongozi wa Simba
Akizungumza na wandishi wa habari Katibu Mkuu wa TFF,
Selestine Mwesigwa alisema kuwa TFF imekutana na Simba na Ramadhani Singano na
kumaliza utata uliokuwepo kwenye mkataba wa mchezaji huo bila kusema ni utata
upi kwani swala la mkataba ni la mchezaji na klabu yake.
Alianza kwa kusema kumekuwa na maneno mengi , kumekuwa na
vichwa vya habari vingi na simu kuhusu swala la mahusiano ya mkataba wa
Ramadhan Singano na Simba na TFF ikaingilia kati swala hilo ambapo kwenye kikao
hicho Simba iliwakilishwa na mjumbe wa kamati ya Utendaji Collin Frich na
Singano alikuwa ameambatana na Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji (SPUTANZA)
“TFF imeamua utata
uliokuwepo kwenye mkataba kati yao na mchezaji Ramadhan Singano umalizwe kwa
kuingia mkataba na pande zote mbili zimeridhia”, alisema Mwesigwa bila kueleza
kwa kina bali alisisitiza kuwa mkataba wa ajira ni kati ya mwajiriwa na mwajiri
Pia Mwesigwa alisema kuwa TFF ina mkataba mama ambao vilabu
na wachazeji wanatakiwa kuufuata kama mfano wakati wa kuingia mkataba na klabu
na kuwataka wachezaji kuelewa mkataba kabla ya kutia saini.
Mwesigwa alisema kuwa wamewaita Simba na Singano ili kutapata
suluhu na siyo kupata mshindi bali
kuhakikisha mchezaji na klabu kila mmoja anapata masilahi yake kwani tofauti ilikuwa
kwenye mkataba kulingana na mkataba mama.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha wachezaji (SPUTANZA), Mussa
Kisoki alisema amefurahi kupatikana
suluhu kati ya mchezaji Ramadhan Singano na Simba na kupongeza TFF kwa
kuingilia kati.
“Nimeridhika kwa matokeo ya mazungumzo ya pande zote mbili
kwani tofauti ndogo tu imegundulika na Messi ni mchezaji halali wa Simba hadi
hapo watakapoingia mkataba”, alisema
Pia alisema kuwa hakuna mahali ambapo mkataba ulikuwa
umeghushiwa bali tofauti ilikuwa ndogo sana na amefurahi kwa upatanishi
uliopatikana kwani
Naye msemaji wa Simba
Hajji Manara alisema yeye hana cha kuongeza kwenye maamuzi yao na kuwasisitiza
wandishi kuheshimu maamuzi ya TFF
“TFF ndio wenye mpira wao na wamefanya maamuzi ambayo
tunatakiwa kuyaheshimu”, alisema Manara huku akiingia kwenye gari .
Kwa upande wake mchezaji Ramadhan Singano alisema kuwa
anamwachia Mungu huku akisisitiza kuwa yeye ni mchezaji huru huku uso wake
ukionyesha kutoridhika na maamuzi.
“Mimi sina zaidi bali namwachia Mungu lakini natambua mimi
ni mchezaji huru kwani mkataba niliokuwa nao unamalizika Julai”, alisema
Singano maarufu kama Messi.
Takribani mwezi mmoja
sasa Ramadhan Singano amekuwa akilalamikia utata wa mkataba uliokuwapo kwenye
mkataba wake na klabu yake ya Simba ambapo yeye alikuwa akidai mkataba wake
unamalizika Julai mwaka huu huku klabu yake ikisema mkataba wake na mchezaji
huyo unamalizika Julai 2016.
No comments:
Post a Comment