
Licha ya kutotwaa Taji lolote Msimu uliopita, Man United imeiengua Bayern Munich na kukamata Nafasi ya Kwanza kwa kuwa ndio Bidhaa ya Biashara yenye thamani kubwa ikikadiriwa kuwa ni Dola Bilioni 1.2 na hii ni kwa mujibu wa takwimu za Washauri mahsusi wa Bidhaa na Fedha, Brand Finance.
Katika Listi iliyotolewa na Washauri hao wa Bidhaa na Fedha, Klabu 6 katika 10 Bora Duniani ni za England.


Brand Finance imesema kuwa kwa kusaini Dili na Wadhamini kama Chevrolet na Adidas, ambao walisaini nao 2014 kwa Dau la Pauni Milioni 750 kwa Miaka 10, ni vitu tosha kuthibitisha thamani ya Klabu hiyo na kwamba thamini yao itapanda zaidi kama ilivyopanda kwa Asilimia 63 tangu 2014.

KLABU 20 BORANA THAMANI YAKE!
1. Manchester United (England): $1206 Milioni
2. Bayern Munich (Germany): $933 M
3. Real Madrid (Spain): $873 M
4. Manchester City (England): $800 M
5. Chelsea (England): $795 M
6. Barcelona (Spain): $773 M
7. Arsenal (England): $703 M
8. Liverpool (England): $577 M
9. Paris Saint-Germain (France): $541 M
10. Tottenham Hotspur (England): $360 M
11 Juventus (Italy): $350 M
12 Borussia Dortmund (Germany): $326 M
13 Schalke 04 (Germany): $302 M
14 AC Milan (Italy): $244 M
15 Everton (England): $228 M
16 West Ham United (England): $209 M
17 AS Monaco (France): $202 M
18 Southampton (England): $183 M
19 Galatasaray (Turkey): $177 M
20 Inter Milan (Italy): $160 M
No comments:
Post a Comment