Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
(TFF) leo limefungua kozi ya makocha wa mpira wa miguu kwa watoto na
vijana kwa nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha vijana wengi wanapata
nafasi ya kufundishwa mpira na kuucheza mpira kuanzia katika umri mdogo.
Akifungua kozi hiyo, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema
ili nchi/Taifa lifanikiwe katika soka ni lazima kuwekeza katika mpira
wa watoto na vijana ambao makocha hao ni sehemu ya uwekezaji huo.
“Tumekua
na mashindano ya Taifa U-13, kikosi cha timu ya Taifa ya U-15 ambayo
inashirikisha vijana wadogo, vijana hao wanapaswa kupata malezi na
mafunzo yenu waalimu ili wafikiapo kuchezea timu za Taifa wawe wamekua
kwenye msingi bora wa kuujua mpira wa miguu” alisema Mwesigwa.
Naye
mkufunzi wa FIFA wa kozi hiyo ya makocha kutoka nchini Ujerumani, Eric
Muller amesema hata ujerumani imefanikiwa baada ya kuwekeza katika soka
la vijana, mwaka 2000 kwenye fainali za Euro nchi yao ilishika nafasi ya
mwisho katika msimamo kundi lao kwa kupata poniti moja, lakini
uwekezaji walioufanya kwenye soka la watoto na vijana umewapelekea
kutwaa Ubingwa wa Dunia mwaka 2014.
Washiriki
wa kozi hiyo ni makocha wa timu za vijana za mikoa yoye Tanzania, ambao
watashirki na timu zao za mikoa katika michuano ya Copa Coca Cola mwaka
huu.
Kozi hiyo ya makocha wa timu za watoto/vijana inayoendeshwa
na wakufunzi wa FIFA, Ulric Mathews kutoka shelisheli na Eric Muller
kutoka nchini Ujerumani itamalizika jumatatu tarehe 29 Juni, 2015.
No comments:
Post a Comment