Marehemu Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ enzi za uhai wake.
MSANII mkongwe wa filamu nchini, Juma
Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ amefariki dunia leo alfajiri akiwa nyumbani
kwake Tandale jijini Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa
kiharusi kwa muda mrefu.
Mwili wa Mzee Kankaa amezikwa leo saa 10 jioni katika makaburi ya Ali Maua jijini Dar es Salaam.
Marehemu
alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa zaidi ya miaka mitatu.
Msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Tandale-Chama jijini Dar.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!
No comments:
Post a Comment