Ripoti toka England zimedai Manchester United wameshaanza mazungumzo na AS Monaco ili wamsaini Beki wa Brazil Fabinho.
Huku
Fulbeki huyo akitaka kuhama, Monaco imeripotiwa kulikataa Dau la Pauni
Milioni 10 la Man United na kutaka walipwe mara mbili.Wakati
huo huo, inasemekana Man United imemchukuwa Wakala kabambe, Jorge
Mendes, ambae ndie huwasimamia Masupastaa kama Cristiano Ronaldo, Jose
Mourinho na kadhalika, ili kuwasaidia kukamilisha Dili ya kumnasa Beki
Nicolas Otamendi ambae Klabu yake Valencia inang'ang'ania kulipwa Pauni
Milioni 35.
Nao Southampton wameiambia Man United kulipa Pauni Milioni 24 ikiwa wanataka kumnunua Kiungo mahiri Morgan Schneiderlin mwenye Miaka 25.
Hadi sasa Man United ndio wako mbele ya Arsenal katika mbio za kumnasa Kiungo huyo kutoka France ambae aliwika kwenye Ligi Kuu England Msimu uliopita.
Hadi sasa Meneja wa Man United, Louis van Gaal amefanikiwa kumnunua Winga wa Holland na PSV Eindhoven, Depay Memphis, ambae ndie Mfungaji Bora wa Ligi Kuu huko Holland.Depay tayari alishatua Old Trafford

No comments:
Post a Comment