Bao
la Dakika ya 36 la Elkin Murillo limeipa Colombia ushindi wa Bao 1-0
walipocheza Mechi ya Kundi C la COPA AMERICA huko Santiago, Chile na
kukatisha wimbi la ushindi la Mechi 11 la Kocha wa Brazil Dunga tangu
achukue wadhifa huo Mwaka Jana.
Mbali ya kufungwa, Nahodha wa Brazil, Neymar, alipewa Kadi Nyekundu na Refa wa Chile, Osses, baada ya Mpira kwisha baada kumbabatiza na Mpira Mchezaji wa Colombia Pablo Armero.
Kadi hiyo kwa Neymar, ambae tayari alishakula Kadi ya Njano mapema kwenye Mechi hiyo na kumaanisha kuikosa mechi ifuatayo ya Brazil kwa vile tayari alishakuwa na Kadi nyingine moja, sasa pia inamaanisha ataikosa Mechi yao ya mwisho ya Kundi C dhidi ya Venezuela na pengine hata zaidi ikiwa itaamuliwa vinginevyo.
Mbali ya Neymar, Carlos Bacca wa Colombia nae alipewa Kadi Nyekundu baada Mpira kwisha baada kumsukuma Mchezaji wa Brazil.
Ushindi huu wa Colombia ni ushindi wao wa kwanza dhidi ya Brazil tangu 1991. Colombia watacheza Mechi yao ya mwisho ya Kundi C dhidi ya Peru huku Kundi hilo likiwa na Timu 3 zilizofungana Pointi 3 kila moja la Vinara wake Venezuela wamecheza mechi 1 tu na Leo watakipiga na Peru iliyo mkiani.

No comments:
Post a Comment