Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, June 5, 2015

FAINALI UEFA CHAMPIONS LEAGUE: JUVENTUS vs BARCELONA KESHO


Barcelona na Juventus Wikiendi hii mojawapo inaweza kuwa Klabu ya 8 Barani Ulaya kutwaa Trebo.Huko Ulaya Klabu inayofanikiwa kuwa Bingwa wa Nchi yake na pia kutwaa Kombe la Nchi hiyo na kisha kufanikiwa kubeba Kombe la UEFA CHAMPIONS LIGI kwenye Msimu mmoja huo huo husemwa imetwaa Trebo.
Hivi karibuni Barcelona waliifunga Athletic Bilbao kwenye Fainali na kubeba Copa del Rey na hiyo inafuatia kuubeba Ubingwa wa Spain wa La Liga.
Nao Juve tayari wameshatia kabatini Kombe la Ubingwa wa Italy baada kushinda Ligi ya Serie A na pia kuchukua Coppa Italia.
Timu hizi mbili zinapambana huko Berlin, Germany kesho kutwa jumamosi Juni 6 kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI na Mshindi atakuwa na Trebo kibindoni.
Wakati Barca ikiwania kutwaa Trebo kwa mara ya pili na kuwa Klabu ya kwanza kufanya hivyo, Juve itakuwa mara yao ya kwanza.
Klabu iliyoanza kutwaa Trebo kwa mara ya kwanza baada ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya kubadilishwa mfumo na jina na kuitwa UEFA CHAMPIONS LIGI ni Manchester United hapo 1999.
Man United bado inaongoza kwa England kutwaa trebo mpaka sasa!
KLABU ZILIZOWAHI KUTWAA TREBO NI:
-CELTIC 1966/67
-AJAX 1971/72
-PSV EINDHOVEN 1987/88
-MAN UNITED 1998/99
-BARCELONA 2008/09
-INTER MILAN 2009/10
-BAYERN MUNICH 2012/13


Mascherano vs. TevezGiorgio Chiellini kuikosa Fainali ya Jumamosi dhidi ya Barcelona kutokana na Majeraha, Hivyo kutocheza mchezo huo kumfanya asikutane na mbaya wake Louis Suarez.

No comments:

Post a Comment