KLABU ya Azam FC imesema kuwa kwa sasa imesitisha usajili wa wachezaji wa ndani baada ya kumchukua mchezaji Ame Ally kutokea Mtibwa Sugar.
Timu hiyo ilimaliza
Ligi Kuu msimu uliopita ikiwa nafasi ya pili na kwa sasa imekuwa ikijipanga kufanya
usajili mzuri kwa lengo la kushinda msimu ujao.
Akizungumza na gazeti
hili jana Msemaji wa Klabu hiyo Jafa Idi Maganga alisema kuwa klabu imefanya
usajili mzuri kwa wachezaji wa ndani na kuwa haina wasiwasi kwa msimu ujao.
Alisema kuwa klabu
inaamini kuwa wapo wachezaji wengine wazuri na waliokuwa wakitaka kusajiliwa na
klabu hiyo lakini kutokana na uchache imewachukua iliyoridhika nao na kuwataka
wengine wenye nia ya kuitaka timu hiyo kujipanga kwa msimu ujao.
"Ndio tumemalizana
na huyu Ame Ally na amejiunga nasi siku chache zilizopita na tumefunga usajili
lakini bado muda na nafasi kwa siku zingine zipo wachezaji
wasitususe"alisema Maganga.
Pia alisema kuwa klabu inasubiria uamuzi wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusiana na kuongeza idadi ya
wachezaji wa kigeni ili kuona ni kiasi gani wanaweza kuongeza wachezaji
wengine.
Alisema kuwa kwa sasa
wameshakamilisha idadi ya wachezaji inayotakiwa ambayo ni wawachezaji watano wa
kigeni na kuwa iwapo ikiruhusiswa kuongeza inawachukua wachezaji ambao
imeshafanya nao mazungumzo.
"Najua kwa
wachezaji wa nje ni watano na kuwa kwa sasa wapo wachezaji kama akina Bamidele
Tope wa Nigeria na wengineo lakini ifahamike kuwa kwa sasa hatuwezi kusema
lolote kuhusiana na mchezaji huyo" alisema Maganga.
Aliongeza kuwa "
hakuna haja ya kumzungumzia huyu kwa sasa kwa kuwa kuna mchakato wa kuangalia
uwezekano wa kuongezea idadi ya wachezaji wa kigeni, ila idadi ikiongezwa basi
wapo wengi".
Klabu tatu kubwa nchini, Yanga,
Azam na Simba zilituma maombi kwa TFF kuomba kuongezewa idadi ya wachezaji wa
kigeni kutoka watano kufikia 10. Na kwa sasa kinachosubiriwa ni maamuzi ya
Kamati ya Utendaji ya TFF.
No comments:
Post a Comment