Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, June 12, 2015

SWANSEA CITY YAMSAJILI AYEW ANDRE, KUVAA JEZI NO. 10

www.bukobasports.comKlabu ya Swansea City inayokipiga Ligi Kuu England imethibitisha kumsaini Mchezaji mpya @AyewAndre na atavaa jezi namba 10 kwa ukamilisho huo wa ujio huo Ligi Kuu katika Klabu hiyo yenye Uwanja unaojulikana Liberty Stadium.
Andre Ayew amesajiliwa kutoka kwenye Klabu ya Marseille. 
Swansea City imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Andre Ayew aliyekuwa anakipiga kunako klabu ya Marseille ya nchini Ufaransa.
Mchezaji huyo sasa anasubiri kuidhinishwa kwa kibali cha Ligi Kuu ya England na cha kimataifa ili aanze majukumu yake mara moja kwenye kikosi hicho cha Swansea.
Ayew mwenye umri wa miaka 25, alikuwa akiwindwa na timu kadhaa za EPL na nyingine za ligi mbalimbali za barani Ulaya, amesaini mkataba wa miaka minne baada ya mkataba wake na Marseille kumalizika.
Ayew atavaa jezi namba10 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Wilfried Bony aliyejiunga na Manchester City mwezi Januari mwaka huu.
 

No comments:

Post a Comment