Katika piga nikupige ya Penati, Timu zote zilifunga Penati zao 3 za kwanza kupitia Lionel Messi, Ezequiel Garay na Ever Banega kwa Argentina huku Colombia wakifunga kupitia James Rodriguez, Radamel Falcao na Juan Cuadrado.
Kwenye Penati ya 4, Muriel akakosa kwa Colombia na Lavezzi kuifungia Argentina na kufanya ngoma iwe 4-3.
Colombia wakafunga Penati yao ya 5 kupitia Cardona na Argentina, wakitakiwa kufunga Penati yao ya 5 ili wasonge, wakakosa Mpigaji akiwa Lucas Biglia na kufanya Bao ziwe 4-4.
Ndipo zikaja nyongeza za Penati moja moja kuamua Mshindi wa papo kwa papo na Colombia kukosa Mpigaji akiwa Zuniga lakini Argentina nao wakakosa ushindi baada ya Marcos Rojo kukosa pia.
Penati iliyofuatia ilipigwa na Colombia lakini Murillo akakosa na akaja Mchezaji mpya wa Boca Juniors ya Argentina, Carlos Tevez, alieanzia Benchi kwenye Mechi hii, na kufunga Penati ya mwisho iliyowapa Argentina ushindi wa Penati 5-4.Kwenye Nusu Fainali, Argentina watacheza na Mshindi kati ya Brazil na Paraguay wanaocheza Leo Usiku.
Nusu nyingine ni kati ya wenyeji Chile na Peru
No comments:
Post a Comment