MKURUGENZI
mpya wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Boniface Wambura ameahidi kuzifanyia kazi
changamoto za ratiba na mapungufu mengine katika kuhakikisha ligi
inachezwa kwa ubora msimu ujao.
Wambura
aliyasema hayo jana wakati akihojiwa na waandishi wa habari, ikiwa ni siku moja
tu tangu kutangazwa kuchaguliwa na
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuchukua nafasi
Alisema
suala la ratiba lilikuwa na malalamiko mengi msimu uliopita hivyo katika
kuhakikisha hajirudii atahakikisha michuano yote ikiwemo kombe la Mapinduzi,
CECAFA, CAF, kalenda ya Fifa, inaingizwa
kwenye ratiba mpya ili kutovuruga utaratibu.
“Tumegundua
kuna michezo mingine kama ya Mapinduzi ambayo tulikuwa hatuiweki kwenye ratiba,
kuna Cecafa, lakini sasa tutayaingiza ili yasitokee malalamiko mengine,”alisema
na kuomba ushirikiano mzuri kwa klabu.
Alisema
jambo kubwa lingine ni suala la viwanja kuhakikisha kuwa vinafanyiwa
marekebisho hasa ule wa Kambarage kuhimiza vyumba viboreshwe kuepukana
malalamiko.
Pia, alisema
kupitia mkutano mkuu wa Bodi ya Ligi utakaofanyika hivi karibuni atarajia
kufanya mazungumzo na klabu zote kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kanuni za
ligi kwa lengo la kuboresha.
Alisema
miongoni mwa changamoto nyingine zilizojitokeza ni baadhi ya timu kuomba kuahirishwa
kwa mechi kwani huwa linavuruga ratiba kwa asilimia kubwa.
Wakati huo
huo, Uongozi wa Yanga umepongeza uteuzi huo mpya na kuhimiza wachaguliwe
wengine watakaoshirikiana na Wmbura katika kusimamia ligi na kuwa bora.
No comments:
Post a Comment