WACHEZAJI 12
wa kimataifa wamiminika Jangwani jijini Dar es Salaam kusaka nafasi ya kuichezea Yanga msimu ujao.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga jerry Muro alisema kati ya wachezaji hao
baadhi wameona wao wenyewe na wengine wamekuja kuomba kusajiliwa Yanga.
“Nia yetu ni
kusajili wachezaji ambao wana ubora watusaidia kufanya vyema katika
michuano ya kimataifa mwakani, lakini
tunaendelea kuangalia kulingana na utaratibu uliowekwa na TFF,”alisema
Alisema ili
kupata nafasi ya kuwasajili wachezaji hao wa kimataifa, tayari wamepeleka
waraka wa mapendekezo yao Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupendekeza idadi
ya usajili kwa wachezaji wa nje ifikie wanane.
Ikiwa
watakubaliwa ombi hilo, alisema wataanza mchakato wa kuwasajili wachezaji
baadhi ambao wana uwezo wa kusaidia timu hiyo kufanya vyema katika michuano
mbalimbali ijayo.
Na ikiwa
hawatakubaliwa wataangalia wachezaji watano wazuri na kuwatumia ilimradi wawe
na uwezo.
Kwa mujibu
wa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bodi ya Ligi Tanzania Boniface Wambura jana,
kila klabu ilipewa taarifa tangu Mei 3, mwaka huu kupendekeza kuhusu kanuni za
ligi na idadi ya wachezaji wanaohitajika.
Wambura
alisema baada ya mapendekezo hayo yatapitiwa na
Kamati ya Utendaji ya TFF na maamuzi yatatolewa kulingana na kanuni za
Shirikisho la Soka duniani (FIFA) na za TFF.
Alisema
maamuzi ya mapendekezo ya wachezaji hayo yafanyika mwezi ujao kwani mwisho wa
klabu kupelekea mapendekezo yao ni mwishoni mwa mwezi huu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment