Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, April 22, 2015

MALINZI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI SAFA


Katika salamau zake kwa Dr. Jordan, Malinzi amesema nchi ya Afrika Kusini imepatwa na pigo kubwa katika tasnia ya mpira wa miguu, kufuatia kifo cha  Mashoeu aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa Kansa ya Utumbo, na  kusema watanzania wako nao pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo.

John Lesiba "Shoe"  Mashoeu aliyezaliwa Disemba 18, 1965 nchini Afrika Kusini, alikuwa ni miongoni wa wachezaji wa nchi hiyo waliotwaa Ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 1996 nchini Afrika Kusini na baadae kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Ufaransa mwaka 1998.

Wakati wa uhai wake Mashoe alipata kuvichezea vilabu vya Giant Blackpool, Kaizer Chiefs, Amazulu na Alexandria United vya Afrika Kusini, na timu Gencleribirligi, Kocaeilispor, Fenerbahce na Busrsapor za Uturuki.

No comments:

Post a Comment