Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, April 22, 2015

BAYERN WAPINDUA KICHAPO NA KUGAWA KICHAPO NA KWENDA NUSU FAINALI UEFA CHAMPIONS LEAGUE BAADA YA KUIFUNGA FC PORTO 6-1

Robert Lewandowski dakika ya 40 tena alifunga bao jingine na kufanya 5-0 baada ya kupata pasi kutoka kwa Thomas Müller.  Hadi mapumziko Bayern walikuwa mbele ya bao 5-0 dhidi ya Timu ya FC Porto. Raha iliyokuwa ikisubiriwa na Mashabiki!! Thomas Müller akishangilia na mwenzake.Thiago Fc Porto Chalii!! Ushindi wa gemu ya kwanza wameivurunda!! hoi!Hii ndiyo raha ya kuwa Meneja!! unashangilia mpaka unajisahau!
Bao la FC Porto lilifungwa dakika ya 73 na Jackson Martínez akipewa pasi na H. Herrera na kufanya 5-1. Xabi Alonso Aliwafunga bao la sita na kufanya mtanange kumalizika kwa bao 6-1 na jumla ya mabao kuwa 7-4. Kwa matokeo hayo Bayern Munich wanakwenda hatua ya Nusu Fainali.
Kocha wa FC Porto hana hamu kipindi cha kwanza tuu kashapagwa kwa kipigo!!Jerome Boateng of Munich and his teammates celebrate scoring their team's second goal
Dakika ya 36 kipindi cha kwanza Thomas Müller aliipa bao la 4 Bayern Munich na kufanya bao jumla kuwa 5-3 baada ya kupata ushirikiano safi kutoka kwa Thiago Alcántara na kufunga bao hilo.
Robert Lewandowski alifunga bao la tatu dakika ya 27 kwa kichwa baada ya kupata krosi safi ya juu kutoka kwa Thomas Müller na kufanya bao kuwa 3-0 dhidi ya FC Porto.Muller hakupimika usiku huu!! Ni yeye na Mashabiki.
Jerome Boateng dakika ya 22 aliwafungia bao la pili Bayern Munich na kufanya 2-0 dhidi ya FC Porto na Agg kuwa 3-3 baada ya kupata pasi kutoka kwa Holger Badstuber. 
Thiago Alcântara kipindi cha kwanza dakika ya 14 aliwapatia bao la kuongoza baada ya kupata mpira kutoka kwa Juan Bernat. UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Robo Fainali-Mechi za Marudiano

Jumanne Aprili 21
Bayern Munich vs FC Porto [Allianz Arena, Munich, Germany] (1-3)
Barcelona vs Paris Saint-Germain [Nou Camp, Barcelona, Spain] (3-1) 

No comments:

Post a Comment