Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, March 4, 2015

SUNDERLAND YAMSIMAMISHA ADAM JOHNSON KWA TUHUMA ZA NGONO NA BINTI MDOGO

KLABU ya Sunderland imemsimamisha Winga wao Adam Johnson baada ya kukamatwa na Polisi kwa tuhuma za kufanya ngono na Binti wa chini ya Umri halali.
Baada ya Polisi kutoa Taarifa kuwa Mtu wa Miaka 27 alikamatwa kwa tuhuma za kufanya ngono na Binti wa chini ya Miaka 16, Magazeti mengi huko Uingereza yalimtuhumu Adam Johnson kuwa ndie Mtuhumiwa kwa kutenda kitendo hicho na Binti wa Miaka 15.
Jonhson, ambae ameichezea England mara 12, alikuwemo kwenye Kikosi cha Sunderland ambacho leo kinacheza na Hull City kwenye Mechi ya Ligi Kuu England lakini baadae aliondolewa na Klabu kutoa Taarifa kuwa amesimamishwa hadi uchunguzi wa Polisi ukamilike.
Johnson ambae sasa yupo huru baada ya Polisi kumuachia kwa dhamana, alianza Soka lake huko Middlesbrough na kisha kujiunga na Manchester City.
Alihamia Sunderland Mwaka 2012 kwa Dau la Pauni Milioni 10 lakini ameshindwa kuonyesha cheche zake za huko nyuma.
Hata hivyo, Mashabiki wa Sunderland wanamthamini sana kwani kwenye Dabi yao na Mpinzani wao mkuu, Newcastle, Johnson amekuwa akipiga Bao muhimu likiwemo Bao la ushindi la Dakika za mwishoni huko St James' Park hapo Desemba 21 Mwaka Jana.
Adam Johnson akiwa amebeba tuzo ya Mwezi kipindi cha nyuma.
Adam Jonson alishachezea England chini ya U21

No comments:

Post a Comment