Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 6, 2015

MOHAMED SALAH AIPA USHINDI FIORENTINA WA KUIKUNG'UTA JUVENTUS MABAO 2-1 COPPA ITALIANA

BAO 2 za Mchezaji wa Mkopo kutoka Chelsea, Mohamed Salah, zimewapa Fiorentina ushindi wa Bao 2-1 Ugenini walipocheza na Juventus katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Coppa Italiana.
Salah, Raia wa Misri, alifunga Bao la Kwanza Dakika ya 11 na Fernando Llorente kusawazisha Dakika ya 24 lakini Salah akawapa ushindi Fiorentina Dakika ya 56.
Mechi za Pili za Marudiano za Nusu Fainali zitachezwa Mwezi ujao.
Paul Pogba akikabwa na Mchezaji Richards kutoka kwa City kwa mkopo sasa akiichezea timu ya Fiorentina
Mohamed Salah alifungua lango kwa kuifungia timu yake bao la kwanza dhidi ya Juventus
Straika wa Juventus Fernando Llorente alisawazisha bao hilo kwa kufanya 1-1
Mchezaji wa Chelsea anayekipiga hapo kwa Mkopo Fiorentina akitokea Chelsea kwa mkopo Salah,aliifungia timu yake ya sasa bao la pili na kufanya 2-1

Wachezaji wa Fiorentina waliungana na kushangilia ushindi wao dhidi ya Vinara Juve usiku

Sala akishangilia kwa kuwapa dole Mashabiki wake kwenye Uwanja huo Juve akipigwa bao 2-1

Mario Gomez akipongezana na Mohamed Salah

No comments:

Post a Comment